Huenda Kafyu ikaendelea hata baada ya Julai Kenya
22/06/2020 23:36 in News

Waziri wa Afya Mutahi Kagwe amesema hajui iwapo marufuku ya kafyu na sitisho la safari za kuingia na kutoka kwenye maeneo ya Nairobi, Mombasa na Mandera yatalegezwa mwezi Julai..

Katika mahojiano na Runinga ya Citizen TV, Waziri Kagwe amesema kulegeza masharti ya kudhibiti Korona kutategemea  na utayarifu wa wakenya katika kukabili virusi hivyo.

Aidha, kanuni zitabuniwa ili kuzingatiwa na washikadau katika sekta mbalimbali kabla ya kufngua shughuli zote

Taarifa hii inajiri  huku Kenya ikiwa imefikisha visa 4,797. Kufikia sasa baada ya watu 59 kuambukizwa katika saa 24 zilizopita.

COMMENTS